WILAYA YA MKINGA WAASWA UMUHIMU WA ELIMU
Kiongozi wa
mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2013 Bw.
Juma Ali Simai ametoa wito kwa wakazi wa wilaya ya Mkinga kulipa kipaumbele suala la elimu kwa vijana
wao na pia amewaasa wanafunzi kusoma kwa bidii na kuepuka vishawishi ili waweze
kufikia malengo yao kimaisha wakati akitoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru kwa wakazi
hao
Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Mhe.Mboni Mgaza akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka
kwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe.Halima
Dendego. Mwenge umepitia jumla ya miradi mitano katika wilaya ya Mkinga yenye thamani ya shilling za Kitanzania
100,495,510
Kiongozi wa mbio za Mwenge Bw. Juma Ali Simai ( wa pili kulia) akikagua
mradi wa Ng’ombe wa Maziwa unaoendeshwa na wanakijiji cha Machimboni
unaofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii Tanzania (TASAF)kwa kushirikiana na wananchi kwa lengo la kuwakwamua wananchi . Kila
mwanakikundi amekabidhiwa ng’ombe mmoja ambaye baadaye humnufaisha kwa maziwa,
mbolea n.k
Trekta hili limezinduliwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Bw.
Juma Ali Simai kwa lengo la kuboresha kilimo cha kisasa katika kijiji cha Mhinduro wilayani Mkinga
Wakazi wa
Mkinga pia wameukaribisha Mwenge wa
Uhuru kwa burudani mbalimbali. Pichani ni Kikundi cha Mapambano eneo la Kasera
wakitoa burudani.
0 comments: