Shida ya maji Mkoani Tanga kubaki historia
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo imesikia kilio cha muda mrefu cha ukosefu wa maji Mkoa wa Tanga na hivyo kuwekeza nguvu zake katika upatikanaji maji. Mwenge wa uhuru umefanikiwa kuzindua na kufungua miradi mikubwa ya maji yenye kusudi la kupunguza na kumaliza kabisa tatizo la maji Mkoani Tanga. Mwenge umezindua mradi wa maji wilaya ya Kilindi wenye thamani ya shiling 263,395,507.74, mradi wa maji wa bwawa la wimba katika kijiji cha Suwa wilayani Handeni unaogharimu shilingi 513,800,000 na mingine kama picha zinavyoonyesha. Miradi yote imetekelezwa kwa nguvu za serikali, wananchi na wadau wa maendeleo nchini.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2013 Bw. Juma ali Simai akifungua mradi wa maji kisima cha Mang’enga wilaya ya Muheza wenye thamani ya shilling 100,000,000 ambao unawanufaisha wakazi wa Muheza kwa maji safi na salama. Pichani ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhe.Subira K. Mgalu akiwa na ndoo ya maji.
Mwanafunzi Fatuma Hassani wa darasa la saba akibebeshwa ndoa ya maji na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Bw. Juma Ali Simai wakati wa ufunguzi wa mradi wa uvunaji maji ya mvua katika Shule ya Msingi Manza wilayani Mkinga ambao utasaidia upatikanaji wa maji salama na kuboresha usafi wa mazingira shuleni hapo. Gharama ya mradi huu ni jumla ya shilingi 11,246,500.
Mkuu wa wilaya ya Lushoto Mhe Majid Mwanga akishuhudia ufunguzi wa maji safi na salama uliofanywa na Kiongozi wa mbio za Mwenge Bw. Ali Simai katika kituo cha walimu Bumbuli (TRC) wilaya ya Lushoto.
0 comments: