Kesho kivumbi mashindano ya UMISSETA kanda ya Kaskazini Mashariki
Hayawi hayawi sasa yanakuwa Mikoa ya Tanga na Kilimanjaro kesho hadi tarehe 06/06/2013 kuchuana ili kupata washindi wa michezo mbalimbali wakatao wakilisha kanda ya kasikazini Mashariki katika mchuano wa Kitaifa ukakaofanyika Kibaha kuanzia tarehe 10Juni, 1013.
Akizungumza ofisini kwake leo ,Ofisa Michezo Mkoa Bi. Digna Tesha amesema tayari wanamichezo kutoka shule za sekondari Kilimanjaro wamekwishawasili kwa ajili ya mpambano huo ambao utafanyika saa mbili asubuhi katika viwanja vitatu tofauti kulingana na aina ya michezo .
Viwanja hivyo ni pamoja na Shule ya Ufundi Tanga ( mpira wa miguu kwa wavulana, mpira wa mikono na riadha), Mkwakwani ( mchezo wa kikapu) na uwanja wa Popatlal ( mpira wa wavu, Netiboli na mpira wa miguu kwa wasichana.
Aidha mara baada ya kupatikana washindi kutakuwa na siku mbili za kuweka kambi ya mazoezi tarehe 07-08/06/2013kujiandaa na mchuano wa Kitaafa na tarehe 09/06/2013 watakuwa safarini kuelekea Kibaha tayari kwa mchuano.
Tunawatakia kheri na mafanikio mema vijana wetu wa Tanga katika mashindano ya Kikanda.
UMISSETA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
0 comments: