UMISSETA kanda ya Kaskazini Mashariki waanza kupata wawakilishi Kitaifa

Michuano ya michezo ya Wanafunzi wa Sekondari kanda ya Kaskazini mashariki (UMISSETA) kati ya  Tanga na Kilimajaro imeanza  rasmi leo  katika viwanja vya shule ya ufundi Tanga. Kanda inajivunia kupata wawakilishi katika michezo ya Riadha na urushaji Tufe. Michezo mingine inaendelea............


 Timu ya Mkoa wa Tanga na Kilimanjaro mchezo wa mikono wakichuana vikali katika kinyanyang’iro cha kupata wawakilishi wa timu ya kanda

Mwanafunzi Martin Swai kutoka mkoa wa Kilimanjaro mmoja wa wachezaji wakataowakilisha kanda ya kaskazini mashariki kwenye mchezo wa kurusha Tufe.  Ameweza kujipatia nafasi hiyo kwa kuwa Mshindi wa kwanza  kikanda.

Wasichana nao hawakuwa nyuma katikamchezo wa  urushaji Tufe. Mwanafunzi Regina Constatino kutoka Mkoa wa Kilimanjaro atawakilisha Kanda ya kaskazini katika mashindano ya kitaifa kwa kuwashinda wenzake kwa point nyingi

Riadha ni miongoni mwa mchezo unaopendwa sana na mkoa wa Tanga umepata wawakilishimmzuri  ambao wataunda timu ya kanda. Mwanafunzi Abdallah S. Abdallah pichani (amevaa kapyura nyekundu) na Asha Kuduga (mita 800),  Halima Mbilu na Isaya Samson ( mita 200) na pia wapo wa mita 100.
Baadhi ya wanariadha  (wasichana) kutoka mikoa ya Tanga na kilimanjaro wakiwa tayari kwa shindano


Written by

0 comments: