Mdahalo wa Wanawake Wilayani Tanga kuhusu Mabadiliko ya Katiba

Wanawake wilayani Tanga wamekutana kwa lengo la  kupata ufahamu zaidi juu ya Rasimu ya Katiba ili kuainisha masuala muhimu kwa ajili ya ustawi wa Wanawake nchini ili hatimaye muainisho huo uingie  katika Katiba mpya ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Mdahalo huu umeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Mti wa Tumaini ( Tree of Hope) wakishirikiana na  shirika la maendeleo la Oxfam la Tanzania. Mdahalo huu ni wa kwanza tangu kutangazwa kwa Rasimu ya katiba

Mhe. Chiku Gallawa  , Mkuu wa Mkoa wa Tanga akifungua rasmi  mdahalo huo akiwa mgeni rasmi. Kutoka kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe.  Halima Dendego, Kaimu RAS Bi. Monica Kinara na  mratibu wa mdaharo Bi. Fortunata Manyereza.
Mshauri mwelekezi wa Masuala ya jinsia Bi. Rose Mjema  akitoa mada juu ya masuala ya unyanyasaji wa kijinsia.
Baadhi ya wajumbe wa mdahalo wa mabadiliko ya katiba
Picha ya Pamoja ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga na wajumbe wa Mdahalo



Written by

0 comments: