Barabara ya Handeni- Korogwe yakamilika
Barabara
yenye kilometa 65 kwa kiwango cha lami inayounganisha Handeni Korogwe na kugharimu
kiasi cha shilling billion 63.199 iko mbioni kuanza kutumika kutokana na ujenzi
wake kuwa katika hatua za mwisho . Barabara hii inajengwa kwa udhamini wa Serikali
ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa asilimia 100% na inategemewa kunufaisha
wakazi wa Mkoa wa Tanga na maeneo jirani.
Akisoma
repoti ya maendeleo ya Ujenzi huo kwa
Mkuu wa Mkoa Mhe. Chiku Gallawa wakati wa ukaguzi , Meneja wa TANROADS Eng.
Alfred Ndumbaro amebainisha changamoto ambazo wamekumbana nazo kuwa ni pamoja
na wananchi kutodhamini mchango wa serikali katika kuwaletea maendeleo kwani
baadhi ya wakazi wamekuwa na tabia ya kuiba baadhi ya vifaa na pia kupitisha
mifugo katika barabara inayojengwa.
Ujenzi
wa barabara hii ulianza februari 2010 chini ya usimamizi wa TANROADS na
kukamilika kwake kutasaidia katika
usafirishaji hivyo kuwapunguzia wananchi kero ya usafiri.
Meneja
wa TANROADS Eng.Alfred Ndumbaro akiwasilisha repoti ya ujenzi wa barabara ya
Handeni – Korogwe
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa akikaguzi ujenzi wa barabara ya Handeni-
Korogwe
Wajumbe
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tanga wakipita katika barabara hiyo
wakati wa ukaguzi
0 comments: