Mkuu wa Mkoa Tanga ashiriki Mazishi ya Mmoja wa Maaskari waliouawa huko Darfur
Marehemu Protonatus Wilbert Msofe ni miongoni mwa
askaria saba mbao wamekufa wakati wakipigania
kutafuta amani huko Darfur. Alizaliwa Mei
21, 1985 na kujiunga na Jeshi la kujenga Taifa mwaka 2006. Hadi mauti inamkuta
Juni 13,2013 marehemu Protonatus alikuwa na cheo cha Private, shujaa huyu alishatunukiwa
medali wakati wa sherehe za miaka 40 ya Jeshi ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake kwa
taifa
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.
Chiku Gallawa akisaini kitabu cha rambirambi nyumbani kwa wazazi wa marehemu maeneo
ya Kange Mkoani Tanga
Mama mzazi wa marehemu
Protonatus, Bi Elizabeth Msofe (mwenye nguo nyeupe) akifarijiwa na Mkuu wa Mkoa Tanga
Mkuu wa Jeshi la Anga Mkoa wa Tanga Kanali L.
Mwakibinga akisoma salamu za rambirambi kutoka kwa Amiri Jeshi Mkuu,Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwa
familia ya marehemu
Baba mzazi wa Marehemu Protonatus, Bw. Wilbert Msofe akipokea salamu za rambirambi zilizokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Baadhi ya Askari wa Jeshi wakitoa heshima kwa Marehemu maeneo ya Makaburi ya Kange Mkoani Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa akiweka shada la maua
Mbunge wa Tanga Mhe. Omari Nundu akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya wakazi wa Tanga.
Baadhi ya ndugu wa karibu wa marehemu na viongozi wa ngazi za juu wa Mkoa wa Tanga.
Baadhi ya umati wa waombolezaji
0 comments: