Kamati ya Bunge ya kudumu ya Miundombinu yatembelea Bandari ya Tanga na Uwanja wa ndege



Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Bw. Fredy John Liundi akipokea wageni wake Mhe. Naibu Waziri  Dk Charles Tizeba na wajumbe wa kamati ya miundo mbinu


Mhe. Naibu Waziri  Dk Charles Tizeba akijibu baadhi ya maswali yaliyoibuliwa na wajumbe wa kamati kuhusu utelekezaji wa bandari ya Tanga baada ya kukamilika  bandari mpya ya Mwambani. Akijibu swali hilo amesema,  serikali haina mpango wa kuitelekeza bandari ya Tanga bali zote zitatumika kwani zina lengo la kuinua uchumi wa nchi

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya miundo mbinu, wataalamu kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa  na bandari  wakiwa kwenye kikao cha majadiliano juu ya maendeleo ya bandari Mkoani Tanga

 

Wajumbe wa kamati ya miundo mbinu ikiwa katika eneo la linalotarajiwa kujengwa Bandari mpya ya Mwambani



Wajumbe wa kamati wakifatilia kwa makini wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya maendeleo ya uwanja wa ndege wa Tanga walipowasili uwanjani hapo


Wajumbe wa kamati wakikagua eneo la uwanja ndege

 


Written by

0 comments: