Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini Wakutana na Waandishi wa Habari Jijiji Dar es salaam Kulitambulisha Kongano la Uwekezaji
Kongano la Uwekezaji Kanda
ya Kaskazini linatarajiwa kufanyika Septemba 26 na 27 mwaka huu katika Hoteli ya Mkonge Jiji la Tanga.
Lengo kuu likiwa ni kukuza Uchumi na Kuongeza ajira Kanda ya Kaskazini. Umuhimu
wa Kongano hili ndio ulilosukuma Wakuu wa Mikoa wa Kanda ya Kaskazini kukutana
leo katika Ukumbi wa kituo cha Uwekezaji ( TIC) na Waandishi wa Habari kutoka vyombo
mbalimbali ili kuweza kuwatangazia Wananchi
na Umma kwa ujumla kuhusu fursa za maendeleo zilizopo katika mikoa hii.
Akizungumza kwa niaba ya
Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini, Mwenyeji wa Kongano hili Mhe. Chiku
Gallawa ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga amesema maandalizi ya Kongano hili yako
katika hatua za mwisho na Mkoa wa Tanga uko tayari kupokea wageni/wawekezaji “
Tunategemea kupokea wageni/wawekezaji zaidi ya 600 kutoka ndani na nje ya
Tanzania na ni imani yetu kwamba kupitia kongano hili hali ya Uchumi katika
Kanda hii utaimarika”
Nao Wakuu wa Mikoa ya
Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga ambayo inaunda Kanda ya Kazkazini wamepata
nafasi ya kunadi fursa za uwekezaji zinazopatikana katika mikoa hiyo. Fursa
nyingi zinapatikana kwenye Kilimo, Utalii, Viwanda, Ufugaji na Madini.
Ni wito
kwa kila mwekezaji kutumia fursa hii kuwekeza katika mikoa hii ambayo imejaliwa
kuwa na rutuba nzuri, hali ya hewa nzuri, madini mbalimbali, mbuga za wanyama
n.k. Kushiriki kwenye Kongano hili jiandikishe kwa fomu maalumu ambayo ipo
kwenye tovuti ya Kanda www.investnorthernzone.go.tz kisha
tembelea fursa za uwekezaji kwa kuchagua Mkoa husika.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Chiku Gallawa akisisitiza jambo katika Mkutano huo
Picha ya pamoja ya Wakuu wa
Mikoa ya Kanda yaKaskazini na baadhi ya viongozi wa TIC. Kutoka kushoto ni Mhe.
Elaston John Mbwilo, mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Magesa .S. Mulongo , Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Mhe. Leonidas E. Gama, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mhe. Chiku Gallawa Mkuu
wa Mkoa wa Tanga. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC)
Bw. Abby Kagomba
0 comments: