Katibu Tawala Mkoa wa Tanga aipongeza timu ya RAS-TANGA kwa Ushindi Michezo ya SHIMIWI
Mashindano ya SHIMIWI
yamemalizika Mkoani Dodoma yalipokuwa yanafanyika kitaifa. Mashindano hayo
yalifunguliwa rasmi na Mhe.Amos Makala
Naibu waziri Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo na kufungwa na Mhe.Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma, timu ya RAS-TANGA imeshiriki katika michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa Miguu , Draft, Karata na
Riadha (wanaume),Kuvuta Kamba wanawake na Bao (Wanawake na Wanaume).
Katika
michezo hiyo Timu ya Mkoa wa Tanga(RAS-TANGA), timu ya Mpira wa Miguu
wanaume ilifanikiwa kufika fainali na kuwa mshindi wa pili kitaifa wakati huo timu ya Wizara ya Elimu ikiwa mshindi wa
kwanza na kwa upande wa mchezo wa Draft , RAS- TANGA imekuwa mshindi wa pili.
Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Benedict Ole Kuyan akiwapongeza
wachezaji wa Timu ya RAS-TANGA wakati waliporejea nyumbani na kombe la ushindi katika hafla fupi
iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Ofisi ya Mkoa.Kulia ni Katibu tawala msaidizi Bi. Monica Kinala na kushoto ni
Mwenyekiti wa Timu Bw. Msafiri Figa
Timu ya RAS TANGA imeleta vikombe viwili nyumbani.
1. Timu
ya RAS-TANGA wakiwa kwenye picha ya pamoja katika ofisi za Mkuu wa Mkoa
0 comments: