Baraza la Madiwani Tanga Kuanza Kupokea Taarifa za Maendeleo ya Kata
Naibu
Meya Mhe.Mzamili Shemdoe akisisitiza jambo wakati wa Baraza la Madiwani. Kulia ni Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Jiji la Tanga Bi. Juliana Malange
Baadhi
ya wajumbe wa Baraza la Madiwani
Baraza la Madiwani Wilaya ya
Tanga limekubaliana na hatua mpya ya kupokea taarifa ya maendeleo ya kila Kata kwa
kila kikao halali cha Madiwani na makubaliano yamefanyika wakati wa kikao cha
kawaida cha Madiwani kilichofanyika tarehe 7/11/2013 katika ukumbi wa mikutano
wa Mipango miji jijini Tanga. Hatua hiyo imepongezwa na wajumbe wa Baraza hilo
kwa kile kinachoaminika kuwa itachochea harakati za maendeleo katika Kata hizo.
Awali Baraza la Madiwani
limekuwa na kawaida ya kupokea taarifa za maendeleo kutoka katika kamati
mbalimbali za maendeleo zikiwemo Kamati
ya Fedha, Kamati ya Mipango miji na mazingira,
Kamati ya Afya, Kamati ya Ukimwi na Maadili na nyinginezo. Mbali na
taarifa kutoka katika Kamati mbalimbali , Serikali imeona kuwa ipo haja ya kupata
taarifa ya kila Kata ili kuchochea nguvu ya maendeleo ya kila Kata.
0 comments: