Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Ahamasisha Umuhimu wa Bima ya Afya
Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw.Benedict Ole Kuyan
akizungumza na wadau wa Bima ya Afya wa Mkoa wa Tanga (hawapo pichani) kwenye
ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkoa wakati wa kikao cha mwaka cha wadau wa Bima
ya Afya
Wadau wa Bima ya Afya Mkoa
wa Tanga wakiwa Kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkoa wa Tanga waliokaa mbele
kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe.Selemani S. Liwowa, Mkuu wa
Wilaya ya Handeni Mhe.Muhingo Rweyemamu na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe.Majid H. Mwanga
Baadhi ya wadau wa Bima ya
Afya Mkoa wa Tanga walioshiriki kwenye
Mkutano wakiwa Ukumbini. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Mhe. Mboni
Mgaza, Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe.Omari Guledi
Wadau wa Bima ya Afya
Mkoani Tanga wamekutana wajadili kwa mapana jinsi ya kuboresha upatikanaji wa
huduma za matibabu katika Hospitali, Vituo vya Afya, Zahanati na Maduka ya dawa
yaliyosajiliwa na Mfuko huu na kuweka mikakati ya kudumu ya kuimarisha huduma
hizo. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa mikutano katika Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa ambapo Katibu Tawala Mkoa wa Tanga
Bw. Benedict Ole Kuyan amebariki Mkutano huo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,
Bw. Ole Kuyan amesema kuwa hadi sasa takwimu zinaonyesha kuwa kufikia Oktoba
30, 2013 hamasa ya kujiunga na Mfuko wa Bima ya
Afya ya jamii Mkoa wa Tanga hairidhishi kwani ni asilimia10% wamejiunga.
“Hali hii inaonyesha kuwa viongozi watendaji na
wadau wengine hatujatimiza wajibu wetu kikamilifu katika kuhamasisha wananchi
hivyo ninatoa wito kwa kila mmoja kuona umuhimu wa kuhamasisha wengine kujiunga
na Mfuko wa Bima ya Afya”
Akipongeza juhudi za Mfuko wa Afya ya jamii, Bw.
Ole Kuyan amesema kuwa wakazi wa Tanga wamefarijika sana kwa kuwepo kwa mradi
wa afya ya mama na mtoto maarufu kama KFW. Mradi huu unatoa mchango mkubwa kwa
Mkoa wa Tanga kuweza kufikia lengo la 4 na 5 la Millennia la kuimarisha afya ya
uzazi na kupunguza vifo vya mama na mtoto. Zaidi ya familia 40,000 zinanufaika
na mradi wa KFW.
Wito umetolewa kwa wanachama wote wa bima ya Afya
kuacha tabia ya kuhujumu kadi zao za matibubu bali wazitunze kadi hizo na
kuacha utaratibu wa kuazimishana kadi za matibabu na hata kuzifanyia biashara.
Nao watoa huduma ya afya wameaswa kutoa huduma kwa
wanachama wa NHIF na CHF sawa na wananchi wengine bila ubaguzi kwa sababu
kumekuwepo na tabia hiyo.
0 comments: