Ufahamu Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa
Mchumi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bi Annunciata .A. Lyimo akiwasilisha mada ya Mkakati wa Matokeo Makubwa Sasa wa Mkoa wa Tanga wakati wa Kikao cha Kamati ya Ushauri Cha Mkoa (RCC).
Kama
sehemu ya juhudi ya kuitoa nchi kutoka kwenye kipato cha chini kwenda kipato
cha kati, kuanzia mwaka wa fedha wa 2013/2014, kwa msaada wa wabia na
maendeleo, Tanzania inatekeleza mpango wa matokeo makubwa sasa; kwa kuitumia
mfumo wa maendeleo uliopata mafanikio makubwa nchini Malaysia
Mfumo
kabambe wa utekelezaji wa maendeleo, ulioelezwa kuwa ni ukuaji wa haraka
unaotokana na wananchi “marathoni” unazingatia maeneo sita ya kipaumbele
yaliyoelezwa katika dira ya maendeleo ya Taifa ya 2025: nishati na gesi asilia,
kilimo, maji, elimu, usafirishaji na utafutaji wa rasilimali. Matokeo Makubwa
Sasa ulizinduliwa na Rais Kikwete, Februari, 2013. Mafunzo ya wiki 8
yaliyoongozwa na wataalamu wa sera ya Malaysia yalitumia uzoefu wa kitengo cha
utendaji wa Menejimenti na utoaji huduma kupanga na kutekeleza mfumo utakaofaa
kwa Tanzania.
Ili
nchi ipate kipato cha kati ifikapo mwaka 2025, ni muhimu kwamba upangaji wa
maendeleo usiwe tena mchakato wa siri kwa watendaji wakuu peke yao na kwamba
wananchi washirikishwe kwa ukamilifu katika kujifunza kuhusu mipango ya
maendeleo na kutoa michango yao itakayozingatiwa. Uwazi na ufanisi ni dhana
zinazoongoza na upunguzaji wa rushwa utakuwa muhimu sana.
Usimamiaji
wa utelekezaji wa matokeo makubwa sasa ni jukumu la kitengo cha utoaji huduma
(kilichopo Ofisi ya Rais). Chombo hiki kinawakutanisha wataalamu na wadau
muhimu wanaoamua na kukubaliana kuhusu vipaumbele na kuviboresha ili viweze
kutekelezeka. Mara nyingi udhaifu wa mara kwa mara umesababisha vipaumbele vya
Tanzania kupuuzwa; matokeo ya haraka sasa inakusudiwa kuhakikisha kuwa kuna
mabadiliko ya mwenendo huo wa zamani, kwa kutayarishwa taratibu
zitakazohakikisha kuwa viongozi wa ngazi za juu wa serikali wanashughulikia
vipaumbele kwa uthabiti zaidi na kuonyesha matokeo na kutimiza malengo
yaliyowekwa. Sehemu hii inakupa taarifa kuhusu sekta sita za kipaumbele za
mpango wa matokeo makubwa sasa.
Katika Mkoa wa Tanga, kipaumbele katika miradi
ya Matokeo Makubwa Sasa kinaelekezwa katika sekta ya maji, Elimu na Mapato.
Mkoa unaazimia kuongeza pato la mtu mmoja mmoja kutoka 886,343 (2011) hadi
1,500,000 ifikapo mwaka 2015 kupitia sekta za uzalishaji mali, kilimo na
ufugajji wa mifugo na nyuki.
Lengo
hilo pia litafikiwa kwa kukuza uchumi na kipato kupitia vikundi vya kiuchumi
vya vijana na wanawake katika maeneo ya mijini na vijijini na pia kuongeza
mapato ya Halmashauri za Wilaya, Miji na Jiji kutoka wastani wa 4% hadi 15%
ifikapo mwaka 2015.
Kwa
upande wa elimu, Mkoa umekusudia kupadisha ufaulu kutoka 32% hadi 60% kwa shule
za msingi na sekondari. Ni Mkakati wa
Mkoa wa Tanga pia kutoa huduma ya maji kwa umbali usiozidi mita 400 kwa kufikia
50% ifikapo 2015.
Mkoa
wa Tanga umejipanga kuendelea kuboresha huduma za kinga na tiba na kutilia
mkazo matumizi ya huduma za bima ya afya CHF kufikia mwaka 2015.
Malengo hayo yatafikiwa kwa bajeti ya shilingi 17,634,463,495
iliyoidhinishwa na Bunge mwaka 2013/2014 na pia kwa kutegemea michango ya wadau
mbalimbali wa maendeleo.
0 comments: