Kata ya Kwamsisi Yapatia Mil 621 Kwa Ajili ya Ujenzi wa Mradi wa Maji
Diwani wa Kata ya Kwamsisi Wilaya ya
Korogwe Mji Nassor Hassan ameishukuru Wizara ya maji pamoja na Benki ya Dunia
kwa kuwapatia ufadhili wa fedha Sh Mil 621 kwa ajili ya kujenga mradi wa maji
ambao ukikamilika utasaida kuondoa kabisa kero ya maji .
Akitoa shukrani zake hapo jana
wakati wa utambulisho wa viongozi wa bodi ya maji kwenye kata hiyo ambao
watakuwa na jukumu la kusimamia ujenzi wa mradi hadi kukamilika kwake na
pamoja na kusimamia huduma ya maji na miundombinu yake isiharibiwe na wananchi
.
Alisema kuwa mradi huo umekuja
wakati muafaka kwani kata hiyo ilikuwa inakabiliwa na
changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa muda mrefu hali
iliyowalazimu wakati mwingine kununua maji ndoo moja kwa kiasi cha Sh 500
kutoka kwa wauzaji wenye magari.
“Tunaishukuru Wizara ya Maji kuleta
mradi wa maji wa kata kumi kwenye wilaya hii na kata hii kwani tulikuwa na
upungufu mkubwa wa maji ,tunapata maji kwenye visima vifupi ambavyo ukichota
zaidi ya ndoo tano vinakauka na inawalazimu kina mama wasubiri kwa muda mrefu
ilikupata maji”alisema Diwani Hassan.
Pia aliitaka bodi hiyo kuhakikisha
inamsimamia mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi kuhakikisha anamaliza mradi
ndani ya miezi sita ya mkataba waliokubaliana na ujenzi unalingana na thamani
ya fedha zilizotumika na sio ubabaishaji.
Hassan alisema kuwa sera ya maji ya
mwaka 2007 imeelekeza kuwa jamii ya vijijini kusimamia utunzaji wa
raslimali ya maji,chanzo cha maji na mazingira ya eneo la chanzo pamoja na
miondombnu iliyopo ili kuhakikisha huduma hiyo inakuwa endelevu na yenye tija
kwa wakajiji wa eneo husika.
Na Amina Omari, Korogwe
0 comments: