Tamasha la Utamaduni Handeni ni Fursa ya maendeleo
Mkuu wa Wilaya Handeni, DC
Muhingo Rweyemamu, amewataka wananchi wa Handeni, mkoani Tanga kulitumia
Tamasha la Handeni kwa ajili ya kutafuta fursa za kimaendeleo
Akizungumza Wilayani Handeni,
Muhingo alisema kutokana na tamasha hilo kufanyika mwisho wa mwaka, Desemba 14,
itakuwa chachu ya kuwaunganisha watu wote, sanjari na kujadili changamoto
zinazoikabiri Handeni na Tanzania kwa ujumla.
Muhingo alisema kuwa tamasha hilo
lina umuhimu mkubwa kutokana na kuandaliwa maalum kwa ajili ya Watanzania kwa
ajili ya kuangalia ngoma na matukio mbalimbali ya kijamii.
“Wakati napongeza kwa dhati
kuandaliwa kwa tamasha hili wilayani hapa, pia nawaomba watu waje kwa wingi
kushuhudia namna gani Handeni imepiga hatua kimaendeleo na kuangalia namna gani
wanaweza kusonga mbele.
“Naamini tutafikia hatua nzuri kwa
kushirikiana na wadau wote, hivyo wale wanaoishi mbali na Handeni pia ni wakati
wao kurudi nyumbani mwishoni mwa mwaka kujifunza mambo ya utamaduni wao,
sanjari na kufanya juhudi za kupiga hatua kimaendeleo,” alisema.
Tamasha hilo linaloandaliwa na
Mratibu wake Kambi Mbwana, hadi sasa limedhamiwa na Phed
Trans, Clouds Media Group, Grace Products, Screen Masters na mtandao wao wa
Saluti5.com, Dullah Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, PLAN
B SOLUTIONS (T) LTD, Country Business Directory (CBD)
na Michuzi Media Group.
Wengine ni duka la mavazi la Chichi
Local Ware, Smart Mind & Arters chini ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa
kupitia kitabu chao cha ‘Ni Wakati Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason
Blog, Jiachie Blog na Taifa Letu.com, huku likipangwa kuanza saa 2 za asubuhi
hadi saa 12 za jioni.
0 comments: