Mkuu wa Mkoa wa Tanga apongeza Halmashauri zilizofanya vizuri Darasa la Saba
Mstahiki
Meya wa Jiji la Tanga Mhe. Omari Guledi akipokea Kikombe cha Ushindi wa
Halmashauri ya Tanga ambayo imekuwa mshindi wa kwanza Kimkoa katika ufaulu wa
darasa la saba 2013. Pongezi hizo zimetolewa wakati wa kikao cha pili cha
Kamati ya Ushauri cha Mkoa kilichofanyika jana kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi
ya Mkoa. Mkoa wa Tanga umekuwa Mshindi wa nne Kitaifa
Halmashauri
ya Korogwe vijijiji imezawadiwa kwa kuonyesha juhudi za ufaulu kwa mwaka 2013 kwa
kuwa mshindi wa tatu Kimkoa tofauti na
nafasi ya 9 iliyoshika mwaka 2012. Pichani ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe
Bw. Peter Mabuga aliyepokea kikombe kwa niaba ya Halmashauri ya Korogwe
vijijini
Mkurugenzi
wa Halmashuri ya Kilindi Daudi Mayaji akipokea kikombe cha ushindi wa Halmashuri iliyoongeza asilimia ya ufaulu
ukilinganisha na miaka ya nyuma. Kilindi imeshika nafasi ya 6 tofauti na mwaka
2012 iliposhika nafasi ya 10
Katibu
Tawala Msaidizi Upande wa Elimu Bw. Chomola Ramadhani akitoa taarifa ya Matokeo ya darasa la saba
Mkoa wa Tanga
0 comments: