Waziri Mwakyembe Akemea Watendaji Wanaokumbatia Biashara za Magendo Tanga
WAZIRI wa Uchukuzi Dk. Harison Mwakyembe amesema
amebaini kuwepo kwa uzembe unaofanywa na baadhi ya watendaji wa Idara za
serikali wanaohusika na shughuli za kila siku katika bandari ya Tanga na
kuwataka waikomeshe haraka.
Amesema uzembe huo unajumuisha utendajikazi wa mazoea unaofanywa na baadhi ya watumishi wa Mamlaka za Bandari(TPA), Mapato(TRA) na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mitandao ya wafanyabishara wanaokwepa kulipa ushuru wa bidhaa pamoja na kupitisha bidhaa haramu zikiwemo Pambe za ndovu na Dawa za Kulevya katika Bandari Bubu 49 zilizoko maeneo mbalimbali ya mkoani Tanga hali anayosema imeeingiza nchi katika hali ngumu ki mataifa.
Ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti katika Wilaya za Pangani, Muheza na Tanga wakati wa ziara yake ya siku moja na kisha kuzungumza na wadau wa bandari waliopo jijini hapa ikiwa ni majumuisho ya ziara yake hiyo iliyolenga kuangalia ustawi wa shughuli na utendaji wa Bandari ya Tanga.
Alisema tija ya bandari ya Tanga ambayo kwa miaka kadhaa sasa inaendeshwa kwa hasara haitaweza kuonekana ili kuiwezesha nayo kujitegemea endeapo watendaji hao wataamua kuendelea kufanya kila mmoja atakavyo kwa maslahi yake binafsi.
“Kuna ujinga ujinga mwingi sana upo hapa Tanga kwa hivyo kama serikali kupitia wizara hii lazima tufanye maamuzi magumu sasa ili kurekebisha hizo dosari zilizopo kwasababu uwepo wa hizi bandari bubu 49 zinaumiza sana uchumi wa nchi”, alisema na kuongeza.
“Kuanzia sasa natangaza rasmi kumalizika kwa honeymoon ya watendaji wa TRA, TPA na Jeshi la Polisi ambao wanashirikiana na wafanyabiashara kuiua Tanga ki uchumi kutokana na harakati zao za kupitisha magendo na vitu haramu”, alisema.
“Inasikitisha sana kuona Tanga ndiyo imekuwa kitovu cha kupokea vitu haramu ikiwemo meno ya Tembo, dawa za kulevya,wahamiaji haramu na bidhaa zisizolipiwa ushuru naomba kama mnanisikia nataka muache mara moja kwasbabu tunajua kila kitu mnachokifanya hapa”.
Dk. Mwakyembe alisema kuanzia sasa atafanya ziara za mara kwa mara ili kuhakikisha mkakati wake huo wa kufichua uozo ulioko kwenye bandari hiyo unafanikiwa ili kuhakikisha bandari hiyo inajiendesha ki biashara kuanzia mwezi Januari mwakani.
“Nataka kuwahakikishia kwamba katika hili hakuna cha TRA wala nani mtu akileta ujinga ili kukwamisha utendajikazi katika wizara ya Uchukuzi nitamfunga bila ubishi kama tulivyowafanyia wenzenu walioko Dar es salaam hapa tutaendeleza na anayedhani hawezi basi kuanzia sasa aanze kutafuta kazi nyingine ya kufanya”, alisema.
Akijibu swali la waandishi wa habari kuhusu mchakato wa ujenzi wa reli ya kutoka Tanga – Kilimanjaro hadi Musoma alisema mazungumzo kati ya serikali na wafadhili yamefikia hatua nzuri ambapo kiasi cha Dola bilioni 3 zinatarajiwa kutatumika kwa ajili ya ujenzi reli hiyo.
“Ujenzi huo utaenda sambamba na uboreshaji njia za reli katika maeneo mbalimbali nchini kwa kuweka vyuma vya uzito kilo 86 kutoka vile vya zamani vyenye uzito wa kilo 56 kwakuwa lengo la serikali ni kuweka miundombinu ya kisasa na yenye ubora mzuri “,alisema.
Aidha, alisema mpaka sasa ujenzi wa reli hiyo umefikia km 600 katika maeneo mbalimbali ambapo ujenzi wa Km. 89 unaendelea katika maeneo ya Malongo hadi Kisarawe ambapo Kampuni China Railways Number II Engineering iliyowahi kujenga reli ya TAZARA ndiyo iliyoonyesha nia ya kuwekeza kwenye ujenzi huo.

Na Anna Makange- Habari leo, Tanga
0 comments: