Watayarishaji wa Vipindi vya Elimu kwa Umma Waaswa Kuwa Wazalendo kwa Kufanya Kazi kwa Weledi
Katika jambo linalotiliwa
mkazo kwa Wanahabari nchini na pia duniani kote ni kufanya kazi kwa weledi. Ukweli
huu umejidhihilisha waziwakati Mkuu wa
Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa akifungua rasmi mkutano wa 97 wa watarishaji
wa vipindi vya Elimu kwa Umma leo unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Tanga Beach Resort Jijini Tanga.
“Naamini mafunzo haya
yatatoa matokea ambayo ni mazuri na kuwaongezea wanahabari uelewa mzuri wa
kuwafikishia wananchi habari ambazo ni sahihi na ambazo zitawasiadia kuinuka
kiuchumi hasa mkijikita katika masuala ambayo yanawagusa moja kwa moja wananchi
“Amesisitiza Mhe. Gallawa.
Aidha ameonya tabia ya
ubinafsi ambayo imo miongoni mwa wanahabari ambao hutafuta habari zenye
uchochezi, kuleta hasira na baadaye kuleta uvunjifu wa amani nchini. Ameongeza
kusema kuwa unahitajika uzalendo katika taaluma ya habari kwani wanahabari wana
nafasi kubwa katika jamii ya kuweza kuihabarisha na kuielimisha jamii.
Naye Mkurugenzi wa Shirika
la Utangazaji Tanzania Bw. Clement Mshana amesema lengo la mkutano huo ambao
utamalizika tarehe 11/12/2013 ni kuwakutanisha watayarishaji wa vipindi vya
elimu kwa umma ili kubadilishana mawazo, uzoefu na kupeana mbinu mbalimbali
zitakazowezesha utayarishaji mzuri wa vipindi vyenye lengo la kuelimisha umma.
Mhe. Chiku Gallawa, Mkuu
wa Mkoa wa Tanga akifungua rasmi mkutano wa watayarishaji wa vipindi vya elimu
kwa umma.
Mkurugenzi wa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) akielezea lengo la mkutano huo
Baadhi
ya washiriki wa Mkutano
0 comments: