Mkuu wa mkoa wa Tanga,Mh. Chiku Gallawa amewaagiza Wakurugenzi Watendaji
wa halmashauri za wilaya mkoani humo kutenga fedha kwa ajili ya kukunua mbegu
ya Mtama ili waweze kuigawanya kwa wakulima msimu huu wa kilimo.
Utekelezaji wa haraka wa agizo amesema utasaidia kuongeza uhakika wa
chakula hasa mtama ambao unauwezo mkubwa kuhimili ukame kuliko zao la mahindi
pamoja na kupunguza tatizo kubwa la njaa linalowakabili baadhi ya wananchi kila
mwaka.
Ametoa mwito huo jana wilayani Handeni wakati akifungua kikao cha kazi kilichojumuisha
watendaji wa sekretarieti ya mkoa, wakuu wa wilaya na maofisa tarafa kwa lengo
la kuharakisha utekelezaji wa mpango wa tekeleza sasa kwa matokeo makubwa(BRN).
Amesema ili kuwawezesha wakulima kuongeza tija kwa kulima mazao yenye
uhakika kuna haja ya kuwahamasisha kwa kuwagawia bure mbegu ya Mtama kuanzia
msimu huu wa Masika badala ya kuwaacha waendelee kulima Mahindi kwa mazoea.
“Wakulima hawana budi kuanza kubadili fikra na mtazamo wao potofu kwamba
zao la Mahindi ndio pekee linaloweza kuwapatia chakula na kuwakwamua ki uchumi
ni Mahindi badala yake waanze kulima Mtama ambao hauhitaji mvua nyingi na hivyo
kuwezesha kupata fedha za kununulia vyakula vingine ikiwemo Mahindi”, alisema.
Aidha, aliwataka Maofisa Ugani kuhakikisha wanatumia vema kipindi hiki
kwa kuwakumbusha wakulima umuhimu wa kuandaa mashamba yao na kutumia mvua za
kwanza za msimu wa Masika utakao anza hivi karibuni kwa ajili ya kupanda mazao
badala ya kusafisha mashamba.
“Maofisa Ugani acheni kukaa ofisini hivi sasa nendeni vijijini
mkawakumbushe wakulima ili waandae mashamba yao kwa ajili ya Msimu wa Masika
ili mvua za kwanza zitakaponyesha wazitumie kupanda mazao yao badala ya
kusubiri inyeshe ndipo waandae mashamba kwa kufanya hivyo watachelewa”, alisema.
Alisema uzoefu unaonesha kwamba idadi kubwa ya wakulima bado wanafanya
shughuli zao kwa kubahatisha na hivyo wanashindwa kutumia vizuri kiasi cha mvua
kinachopatikana kila msimu hatua inayoathiri uzalishaji wa mazao ya chakula.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mh.Muhingo Rweyemamu
aliyekuwa mwenyeji wa mkutano huo akimkaribisha Mkuu wa Mkoa kufua Mkutano.
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Tanga
wakifuatilia mjadala katika mkutano huo.Toka kushoto ni Wah.Mboni Mgaza
(Mkinga),Subira Mgalu (Muheza), na Hafsa Mtasiwa (Pangani).
Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha Sekretariet ya Mkoa
waliohudhuria mkutano huo katika ukumbi wa Hill town View Hotel mjini Handeni.
Cras sed felis et risus mattis condimentum. Maecenas ut lacus vel nibh iaculis commodo. Pellentesque vel sapien eu dui suscipit sodales vestibulum id erat.
0 comments: