Watumishi Kutoka Secretarieti Ya Mkoa wa Tanga Washiriki mafunzo ya Zimamoto na Uokoaji
Watumishi
wa kada mbalimbali kutoka katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga wamepatiwa mafunzo juu ya uokoaji wakati wa majanga ya moto jana katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji . Madhumuni ya mafunzo hayo ni kuwawezesha watumishi hao kujifunza na
kutafakari njia za kuzuia majanga ya moto
kutokea na endapo yatatatokea waweze
kujua taratibu za kiusalama za kukabiliana na hali hiyo. Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji ni Idara ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani na
inaendesha shughuli zake chini ya sheria
ya Zimamoto na Uokoaji “ The Fire and
Rescue Force Act No . 14 ya mwaka 2007.
Koplo Musa Msengi, Afisa wa Mafunzo kutoka Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji ( kulia) akitoa maelezo kwa Watumishi kutoka Secretarieti ya Mkoa wa
Tanga juu ya matumizi ya vifaa vya
Zimamoto ( Fire extinguishers) kwa moto
mdogo unaochukua dakika 0 hadi 3 . Kulia ni Koplo Grace J. Silayo na Koplo
Diriki Loshashi (katikati) ambaye ni
Mkuu wa Mafunzo Kutoka Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji Mkoani Tanga
Koplo Musa Msengi akielezea matumizi ya
kifaa cha zimamoto kinachoitwa (Hose reel) kwa lugha ya kitaalamu ambacho hutumika
kuzimia moto wa wastani unachukua dakika
4 hadi 9
mafunzo vitendo ya kifaa cha "Hose reel"
Watumishi wa kada mbalimbali kutoka Secretarieti ya Mkoa wa Tanga wakisikiliza kwa makini wakati wa mafunzo ya nadharia ya uokoaji wakati wa majanga ya moto ambayo yamefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Visima maalumu kwa ajili ya maji yanayotumika
wakati wa uokoaji ( Hyhdrants) ni muhimu
kutunzwa na kuenziwa . Pichani , Koplo Msengi akionyesha mfano wa
matumizi ya kisima kilichopo katika eneo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Mwenye suti
nyeusi ni Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Salum M. Chima (Alhaj)
0 comments: