Ziara Ya Kamati Ya Maudhui Kutembelea Vituo vya Radio na Television Mkoani Tanga



  Ujumbe wa Kamati ya Maudhui ukimtembelea Mkuu Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa (Katikati) ofisini kwake mara baada ya kuwasili katika Mkoa wa Tanga  kwa ziara ya kutembelea vituo vya Redio na Televisheni mapema wiki hii. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui Bi. Magret Munyagi ambaye amemweleza Mhe. Gallawa nia na lengo la ziara hiyo kuwa ni kukumbushana kanuni na taratibu za uendeshaji vituo vya Radio na Televisheni nchini.
Moja kati ya kanuni hizo ni kutumia vyombo vya habari kwa lengo la kujenga na kuleta maendeleo badala ya kuwa chanzo cha uchochezi  na uvunjifu wa amani, matumizi ya lugha ya taifa ( Kiswahili) n.k. Baada ya ziara , Kamati inategemea  kuwa na Warsha ya siku moja na wadau wa Redio na Television ambayo itafanyika siku ya Ijumaa 13 Juni, 2013 katika hoteli ya Regal Naivera Jijini Tanga.
Timu ya Kamati ya Maudhui, Viongozi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mwakilishi kutoka Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni


Bi. Magret Munyagi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari  wa Tanga uliofanyika katika ukumbi wa kitu  cha Walemavu ( YDCP) akiutaarifu Umma lengo la ujio wa ziara ya Kamati hiyo. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi  Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Fredrick Ntobi na kulia ni Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa TCRA Eng. Annet Matindi


Naibu Mkurugenzi  Utangazaji wa TRCA Bw. Fredric Ntobi akifafanua jambo wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Tanga
Bw. Innocent Mungi, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) akifafanua jambo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Maudhui ofisini kwake. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui Bi Magret Munyagi na kushoto ni Bw.Abdul Ngarawa. Mstari wa nyuma kulia ni Bw.Yusuf Nzowa na kushoto ni Joseph Mapunda





Written by

0 comments: