Hawa Ghasia Afungua Rasmi Maadhimisho ya Serikali Za Mitaa Kitaifa 2014, Mkoani Tanga



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Hawa Ghasia ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao wa viongozi wa Serikali za Mitaa. 

Hayo yamesemwa wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya Serikali za Mitaa  yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Tangamano Jijini  Tanga  yenye kauli mbiu " Katiba Mpya izingatie kuwa Serikali za Mitaa ni msingi wa Maendeleo Endelevu: Mwananchi Shiriki katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa"


 Maadhimisho hayo yataambatana na ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo katika Halmashauri za Tanga, Kongamano lenye mada mbalimbali zihusuzo shughuli za serikali za mitaa na Waziri Mkuu kufanya kikao na Mameya wa Majiji, Manispaa na Wenyeviti wa Halmashauri za Mji na Wilaya Tanzania. 

Kilele cha Maadhimisho  haya kitafanyika Julai Mosi mwaka huu. Mwaka jana , Maadhimisho hayo yalifanyika  Mkoa wa morogoro.
 Viongozi wa Kitaifa na Mkoa wakati wa ufunguzi

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa akitoa salamu za Mkoa 


Mkuu wa wilaya ya Tanga, Mhe Halima Dendego akitoa utambulisho

Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga akiongea wakati wa Ufunguzi


Mhe. Hawa Ghasia alipata wasaa wa kutembelea mabanda ya maonesho ya Halmashauri za mbalimbali. Pichani ni Bi. Merry Lyon ambaye ni Mtaalamu wa Kilimo cha mbogamboga kutoka Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga akitoa ufafanuzi 
 




Written by

0 comments: