Serikali Yaitaka TANROADS Kuwa Wakala Bora wa Barabara Barani Africa
Serikali
imeitaka TANROADS kuwa Wakala Bora wa barabara Barani Africa kwani secta ya
barabara inatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Mkoa na nchi kwa ujumla. Ni
jukumu la TANROADS kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia kanuni na sheria za
nchi.
Hayo
yamesemwa na Mgeni rasmi Mhe. Hafsa Mtasiwa , Mkuu wa Wilaya ya Pangani ambaye amemwakilisha
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa alipokuwa akisoma hotuba wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa nne wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara (TANROADS)
linaloendelea katika ukumbi wa hoteli ya
Tanga Beach Resort Jijini Tanga leo na kumalizika tarehe 18Juni, 2013.
Naye
Eng. Mfugale, ambaye ni mwenyekiti wa baraza la Wafanyakazi anaelezea lengo la
Baraza la Wafanyakazi ni kuwaleta
wajumbe wote pamoja katika kutafakari na kujipima ni kwa jinsi gani malengo
yamefikiwa na kwa jinsi gani wajipange kwa mwaka mwingine.
Sehemu
ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS
wakiimba wimbo wa
mshikamano
Eng. Patrick MFugale,
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS akimkaribisha mgeni rasmi
Wajumbe wa Baraza la
Wafanyakazi wa TANROADS
Bi.Hawa
Mmanga, Mwenyekiti wa body ya Wakurugenzi ya TANROADS akitoa neno la shukurani
Picha
ya pamoja ya Mhe. Hafsa Mtasiwa na Wajumbe wa baraza la Wafanyakazi
0 comments: