SSRA Yatoa Semina Kwa Wadau Wa Mifuko Ya Hifadhi za Jamii Mkoani Tanga



Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (SSRA) inatoa semina  juu ya  uelewa wa shughuli  na majukumu ya Mamlaka hiyo kwa wadau wa mifuko ya hifadhi ya Jamii  Mkoani Tanga. Mafunzo yameanza Juni 23, 2014 na yataendelea kwa muda wa siku nne.

Pichani ni  Bw. Salum M. Chima ,Katibu Tawala  Mkoa wa Tanga akifungua rasmi semina  iliyotolewa kwa  Makatibu Tawala Wasaidizi kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Tanga, Makatibu Tawala na Maafisa Utumishi kutoka Wilaya za Tanga  katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Bw. Chima amewataka washiriki wa semina kuitumia elimu waliyoipata  kwa maslahi ya maendeleo na hatimaye kuwa wakala wazuri wa kujiwekea akiba itakayo wasaidia wakati wa majanga.

Wadau wengine ambao watanufaika na wafunzo hayo ni Polisi na wadau kutoka Chama cha Wafanyakazi (TUCTA). SSRA iliundwa kwa sheria Na. 8 ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2008 na kufanyiwa marekebisho ya sheria  Na. 5 ya Mwaka 2012 kwa lengo la kusimamia na kudhibiti Sekta ya Hifadhi ya Jamii. Mamlaka  imeanza majukumu yake tangu mwaka 2010.
  Bi Amina S. Ally, Mwakilishi kutoka Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji  cha SSRA akitoa maada juu ya majukumu ya Mamlaka hiyo kwa washiriki (hawapo pichani)

Washiriki kutoka makundi mbalimbali wakati wa semina

Bw. Robert Mtatiro, Afisa Utumishi kutoka Sekretarieti ya Mkoa Tanga akichangia mada  wakati wa majadiliano

Bi. Samina A. Gullam  akichangia mada wakati wa majadiliano
Dr Carina Wangwe ambaye ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa SSRA akifafanua jambo wakati wa semina
 Bw.Peter Mabuga, Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe akitoa neno la shukrani

Bi. Monica Kinala , Katibu Tawala Msaidizi- upande wa Miundo mbinu kutoka Secretarieti ya Mkoa Tanga akifunga rasmi  semina
 Picha ya Pamoja ya mgeni rasmi na washiriki wa semina


Written by

0 comments: