Chiku Gallawa Asihi Mshikamano Kupunguza Kasi Ya Maambukizi Ya Ukimwi Mkoani Tanga
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Chiku Gallawa amewataka
wakazi wa Tanga na Taifa kwa ujumla
kuonyesha mshikamano na kuendelea
kuhamasishana ili kupunguza kasi ya maambukizi mapya ya Ukimwi.
Hayo ameyasema kwa uchungu wakati akifungua rasmi kikao
cha wadau wa UKIMWI wa Mkoa wa Tanga kilichofanyika mwishoni mwa wki katika
ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jijini Tanga.
“Hali ya takwimu ya utafiti wa 2011/12 wa maambukizi ya Ukimwi kitaifa ni asilimia 5.1 na kwa Mkoa wa Tanga ni asilimia 2.4, hali
ambayo inaonyesha kuwa kati ya watu 100 watu 2 wana maambukizi ya VVU. Hali hii
inatishia maendeleo ya jamii kwa Mkoa wa Tanga”
Mtazamo waKitaifa na
kimataifa kwa sasa ni kutokomeza kabisa maambukizi mapya ya VVU, unyanyapaa na
vifo vinavyotokana na UKIMWI. Ni wajibu wa kila mmoja kushikamana ili
kutokomeza ugonjwa huu hatari.
Bw. Ramadhani Kaswa, Katibu
Tawala Msaidizi – Mipango akichangia mada wakatu wa kikao
Wajumbe wanawakilisha makundi mbalimbali katika jamii Jijini Tanga wakisikiliza kwa makini
0 comments: