Rais Kikwete Azindua Nyumba Za Gharama Nafuu Kwa Watumishi Wa Halmashauri Ya Wilaya ya Mkinga
Mhe. DktJakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania akiwa na viongozi wa kitaifa, Mkoa na Wilaya ya Minga mwishoni mwa
wiki wakati akizindua rasmi nyumba mpya za gharama nafuu ambazo zimejengwa na Shirika la nyumba (NHC)
kwa ajili ya watumishi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Mkinga Mkoa wa Tanga zinalenga
kupunguza kero ya makazi kwa watumishi hao .
Mhe. Kikwete amekuwa kwenye ziara ya siku moja
katika Wilaya hiyo ambapo amepata fursa ya kuongea na wananchi katika mkutano
wa hadhara na kisha kuwafuturisha eneo
la malamba jeshini.
Mkurugenzi
wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Benedick Kilimba akimuonyesha Rais Jakaya Kikwete michoro ya
nyumba ambazo Shirika hilo imezijenga Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Mkoani
Tanga wakati wa uzinduzi wa mradi wa
nyumba za gharama nafuu kwa watumishi wa Wilaya hiyo jana
Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa nyumba mpya za watumishi wa halmashauri ya
Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga
zilizojengwa na Shirika la nyumba la Taifa (NHC), kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi, nyumba na Maendeleo na
Makazi, George Simbachawene na kushoto
ni Mwakilishi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba na watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku
Gallawa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria kupokea mashine mpya na za kisasa 40 za kufyatulia matofali (Hydraform) ambazo Shirika la nyumba
la Taifa (NHC) imezipa Halmashauri zote
za Mkoa wa Tanga ili kuwapatia vikundi vya vijana kuanzisha mradi wa ufyatuaji wa matofali na
kuweza kujikwamua kimaisha. Picha na Salim Mohamed-Mwananchi
0 comments: