Mkoa Wa Tanga Wajipanga Kutokomeza Vifo Vya Wamama Wajawazito
Serikali kwa kushirikiana na wadau wa afya imechukua
hatua mbalimbali katika kuboresha huduma ya afya hususani katika kupunguza vifo
vya akina mama wajawazito.
Hayo yamesemwa
na Mkuu wa Mkoa waTanga Mhe. Chiku Gallawa leo wakati akifungua Kikao cha mwaka
cha tathmini ya namna ya kupunguza vifo vya akina mama na watoto chini yamiaka
mitano kilichohusisha Wakuu wa Wilaya za Tanga, Wakurugezi na Waganga wa Wilaya
kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa.
Amesema kuwa tatizo linalowakabili akinamama wajawazito
na watoto chini ya umri wa miaka mitano halina budi kupungua ikiwezekana
kuzibitiwa kabisa. Pia Mhe Gallawa ameshauri kuwepo dawati la lishe kwa kila Halmashauri ili kusaidia akinamama.
Hatua zinazochukuliwa na Serikali ni pamoja na kutoa
mafunzo kwa watendaji, kuongeza ajira za watumishi wa kada za afya na kuongeza
upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.
Wakichangia mada kwa wakati tofauti, watumishi kutoka kada ya afya
wameishauri Serikali kuhakikikisha kuna kuwepo na vyumba vya kupumzikia
wamamama wajawazito (Maternity home) kwenye vituo vya afya wakati wakisubiria
kujifungua ili kupunguza uwezekano wa wamama hao kujifungulia majumbani/njiani.
Wananchi pia wameonywa kuacha tabia ya kuzipa nafasi
mila na desturi ambao hupelekea ucheleweshwaji wa mama wajawazito kufikishwa
katika vituo vya afya kwa mfano mama kutoa taarifa ya uchungu katika hatua ya
mwisho .
Mratibu wa Chanjo kutoka hospitali ya Rufaa ya Bombo Bw. Seif Shaibu akitoa mada inayohusu masuala ya chanjo
Katibu Tawala Mkoa
Tanga Bw. Salum M. Chima ( Alhaji ) akichangia mada
Washiriki wa Kikao
Mhe. Subira Mgalu, Mkuu wa Wilaya ya Muheza akichangia
mada
Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Tanga Dr. Asha Mahita akitoa
ufafanuzi wa nini kifanyike ili kuboresha huduma za afya katika hospitali na
vituo vya afya Mkoani Tanga
0 comments: