Mkutano Wa Ushawishi Na Utetezi Wa Uboreshaji Masuala Ya Lishe Kwa Mkoa Wa Tanga, Wadau Wa Afya Waonywa Vyakula Visivyo Na Virutubisho
Shirika la Elimu Duniani (WEI) kwa kushirikiana na Shirika
la Misaada la Marekani la USAID limefanya Mkutano wa siku moja uliyoshirikisha
Wakuu wa Wilaya , Wakurugenzi na Wenyeviti wa Halmashauri za Miji na Wilaya za
Tanga na Maafisa lishe iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Lengo ni
kukumbusha sera, miongozo na mikakati ya Serikali juu ya lishe na umuhimu wa kuingiza maswala ya lishe
katika mipango na bajeti ya kila Halmashauri . Pichani Mhe. Chiku Gallawa , Mkuu wa Mkoa wa Tanga
akifungua rasmi Mkutano huo mapema jana
Bi .Grace Muro, Mratibu wa ushawishi na utetezi kutoka shirika la elimu (WEI)“ World
Education Inc” akizungumza wakati wa mkutano. Waliokaa kulia ni Mhe. Chiku Gallawa , Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Katibu Tawala Bw. Salum M. Chima (Alhaji) na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Dr Asha Mahita.
Bw. Francis Modaha Mtafiti na Mkufunzi ambaye ni mwakilishi
kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akiwasilisha tathmini ya tatizo la Utapiamlo nchini hususani Mkoa wa
Tanga
Bw.Magawa N. Abdallah, Meneja kutoka Ofisi ndogo ya
Shirika la Elimu Duniani (WEI) Mkoani Tanga akichangia mada
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano kutoka Wilaya za Tanga
Picha ya pamoja ya Mhe. Chiku Gallawa , Mkuu wa Mkoa Tanga na Washiriki wa
mkutano
0 comments: