Serikali Yatenga Bilioni 21 Kumaliza Tatizo la Vitabu Nchini
Rais Jakaya Kikwete amesema serikali imetenga kiasi cha
sh. Bilioni 21 katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2014/2015 kwa ajili ya
kumaliza tatizo la upungufu wa vitabu kwenye shule za sekondari.
Kauli hiyo ameitoa wakati akihutubia wananchi wa kata ya Kimbe baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye maabara ya masomo ya sayansi ya sekondari ya kata hiyo ambapo ujenzi wake utagharimu jumla ya sh. Milioni 135 hadi kukamilika.
Mpaka sasa ujenzi wa maabara hiyo ya masomo ya Fizikia, Kemia na Baiologia ulioanza mwaka jana umegharimu jumla ya sh milioni 59 ambapo kati ya hizo mchango wa wananchi ni sh. Milioni 47.4, halmashauri sh milioni 12.5 na kiasi kilichobaki ni mchango wa serikali kuu ambapo ujenzi huo uunatarajiwa kukamilika baadae mwezi Novemba mwaka huu.
Amesema fedha hizo zimeongezwa ili kuendea kukabiliana na uhaba wa vitabu vikiwemo vya mazomo ya Baiolojia, Kemia, Fizikia na Hisabati ili kuwawezesha wanafunzi wanaosoma katika shule za sekondari hususan za Kata kujifunza masomo ya sayansi.
“Katika mwaka ujao wa fedha tumeamua kuongeza fedha tunazotenga kwa ajili ya ununuzi wa vitabu na lengo hasa la serikali ni kupunguza tatizo lililopo sasa pamoja na kuboresha mazingira ya kujifunzia”, alisema.
Aliongeza, “ Lengo la kuhakikisha la kuongeza msisistizo katika kuboresha mazingira ya utoaji elimu hasa kwa kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi ni kuwezesha kata kupata wataalam wa wenye ujuzu katika fani za sayansi ikiwemo Afya, Uhandisi, Madakrati ambao watasaidia kuchochea maendeleo ya jamii husika na taifa kwa ujumla”, alisema.
Aidha, amesema serikali inatambua tatizo la uhaba wa nyumba za walimu na kwamba tayari imetenga kiasi cha sh. Milioni 500 kwa kila halmashauri nchini ili kupunguza tatizo hilo.
“Kwa kutambua umuhimu wa shuele za sekondari za kata serikali imeamua kutenga sh. Milioni 500 kwa kila halmashauri ili kuendeleza mpango wa ujenzi wa nyumba za walimu ambao utaboresha mazingira yao ya kazi na kuongeza uhakikia wa walimu shuleni”.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilindi, Daudi Mayeji akizungumzia utekelezaji wa Mpango wa dharura wa serikali wa kukabiliana na uhaba wa maabara alisema kwa Kilindi tayari halmashauri imenunua maabara nne zinazotembea (Mobile Laboratory) zenye thamani ya sh. milioni 10 mwaka huu wa fedha.
Awali Mbunge wa jimbo la Kilindi, Beatrice Shelukindo alimweleza rais kuwa tatizo kubwa linalowakabili wananchi wake ni bei ndogo ya mazao hasa Mahindi ambapo wakati wa msimu wa mavuno debe moja linauzwa kwa sh. 2,400.
Akijibu ombi hilo rais alisema atawaelekeza wakala wa taifa wa ununuzi wa mazao wenye ofisi zao wilayani Handeni (NFRA) kununua mahindi ya wakulima wa wilayani Kilindi ili kuwawezesha kujikwamua ki uchumi. Habari na Anna Makange- Habari Leo Tanga

0 comments: