Ziara Ya Mhe. Dkt Jakaya Kikwete Wilayani Kilindi
1
Mhe. Dkt.Jakaya Kikwete , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika
ziara ya kikazi ya siku mbili Wilayani Kilindi mwanzoni mwa wiki ambapo amezindua ; kufungua na kuweka mawe ya
msingi katika miradi mbalimbali.
Lengo la
ziara hiyo ni kukagua shughuli za maendeleo na pia kupata kufahamu juu ya mafanikio na changamoto katika Wilaya hiyo.
Pichani Mhe. Dkt Jakaya Kikwete mara baada ya kuweka jiwe la msingi ktatika
vyumba vya maabara katika shule ya sekondari ya Kimbe kata ya Kimbe Wilayani kilindi . Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilindi
Mhe. Sulemani Liwowa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa.
Mhe.
Dkt Kiwete akihutubia wananchi kata ya Kimbe Wilayani Kilindi
Sehemu ya wananchi wakati wa mikutano ya hadhara
Mhe.
Jakaya Kikwete akizindua jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi.
Kushoto ni Mhe. Beatrice Shelukindo, Mbunge wa Jimbo la Kilindi .Kulia ni Bw. Daudi Mayeji, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi na Mwenyekiti wa
Halmashauri Bw. Musa Semdoe
Mhe.
Jakaya Kikwete akikabidhi pikipiki 20 kwa Watendaji wa Kata za Kilindi. Pichani
ni mmoja wa watendaji hao akipokea ufunguo wa pikipiki ambapo amewakilisha watendaji wenzake
Mhe.
Jakaya Kikwete akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa Kwadiboma wakati akizindua
mradi wa maji wa vijiji kumi katika kata ya kwadiboma wilayani Kilindi
Mhe. Dkt Jakaya
Kikwete akimkabidhi Kombe ambalo linatarajiwa kushindaniwa katika ligi ya Wilaya ambayo imepewa heshima ya jina la Kikwete Cup itakayochezwa mapema mwaka huu kwa Katibu wa TFF Wilaya ya Kilindi Bwana Omari Javu
wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Songe Wilayani Kilindi- picha na Osca Assenga Tanga
0 comments: