Ufunguzi Gallawa Cup 2014


Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Chiku Gallawa amefungua rasmi Mashindano ya Mpira wa Miguu yenye jina la Gallawa Cup mwishoni mwa wiki  katika viwanja vya Mkwakwani jijini Tanga na yanaendelea hadi fainali Julai  mosi 2014.  Mashindano haya yana lengo la  kukuza mahusiano mema na kukuza vipaji vya wachezaji wa soka ambayo ni mkusanyiko wa vijana kutoka Wilaya saba za Tanga ambazo ni Tanga, Mkinga, Muheza, Pangani,Kilindi, Korogwe na Handeni. Mashindano haya ni ya kwanza kwa Mkoa wa Tanga.

Awali mashindano hayo yameanzia ngazi za vijiji na kata na hatimaye mashindayo ya wilaya yaliyopewa majina ya wakuu wa Wilaya. Mashindano haya yanategemea kuendelea kwa kila mwaka.  Wadhamini wa mashindano haya ni Benki ya NMB ambayo imetoa ufadhili wa jezi tisa , mipira 10 ambavyo vimegawiwa kwa timu zote na pia imetoa vikombe vitatu kwa washindi.
 Wakati wa maandamano
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Halima Dendego  akitoa utambulisho kwa viongozi wa Mkoa na Wilaya.

 Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania  tayari kutoa msaada wa kiafya
Viongozi mbalimbali wa Mkoa na Wilaya
Digna Tesha , Afisa Michezo Mkoa wa Tanga akitoa taarifa juu ya mashindano hayo
Wakuu wa Wilaya wakifanya ukaguzi wa timu. Kulia ni Mhe. Hafsa Mtasiwa, Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mhe. Mboni Mgaza, Mkuu wa Wilaya ya Mkinga (katikati) kushoto ni Mhe. Sulemani Liwowa, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa akifunga goli kuashiria ufunguzi wa mashindano hayo.



Written by

0 comments: