Kukamilika Kwa Jengo La Makao Makuu ya Halmashauri Ya Mkinga Ni Faraja Kwa Wananchi
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Mkinga kuanza
kufanya kazi kwa ufanisi na kutoa huduma kwa wananchi kwa ukaribu hii ni baada
ya ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Halmashauri kufikia hatua nzuri.
Akiweka jiwe la msingi wa ujenzi wa jengo hilo ambalo
linatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi za Kitanzania Bilioni
4,402,166,504/=, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2014 kitaifa amepongeza
juhudi za Serikali katika kuwaletea wananchi wake maendeleo . pia ametoa onyo kwa baadhi ya wananchi wanaobeza juhudi za Serikali katika kuwaletea wananchi wake maendeleo.
Katika miradi yake, Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga imekuzindua tovuti yake
yenye anuani www.mkinga.go.tz
ambayo inatoa fursa kwa wakazi wa Mkinga na wananchi kwa ujumla kufahamishwa na
kuelimishwa shughuli, mikakati na fursa za maendeleo katika Wilaya hiyo.
Zubeda Juma ambaye ni Bibi Shamba Kata ya Gombezi
kijiji cha Vunde akitoa maelezo kwa Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa 2014 Bw.Hamza Ibrahim Mahmoud kutoka Mjini
Magharibi mara baada ya kukagua mradi wa
shamba la mbegu bora ya nuhogo aina ya kiroba. Mradi huo utanufaisha wakulima kuuza mbegu na kupata
chakula cha familia na unaghaimu kiasi
cha shilingi milioni 2,674,000/=
Bi.
Rachel Stephen Kassanda akizindua rasmi tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mkinga
yenye anuani www.mkinga.go.tz
Jengo
la ofisi ya Kata Parungu Kasera Wilayani Mkinga lililowekwa jiwe la msingi na Kiongozi wa mbio
za Mwenge kitaifa 2014 Bi. Rachel
Kassanda
Mwenge haubagui rangi , kabila wala itikai za kisiasa
0 comments: