Pangani Sasa Kunufaika na Kilimo cha Muhogo
Mradi wa kituo cha usindikaji Muhogo wenye thamani ya
shilingi milioni 56,475,000/= katika
Kata ya Madanga ambao uko unatarajiwa kuwa soko la uhakika kwa wakulima wa Kata ya Madanga pamoja na kata jirani.
Akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa jengo la kituo
hicho Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2014
Bi. Rachel Stephen Kassanda amewaasa Wakazi wa Madanga kutumia fursa hiyo adimu
kwa kuzalisha kwa wingi zao la Muhogo ili kujikwamua na hali ngumu ya maisha.
Ujenzi wa kituo hiki ni nia ya serikali katika kuweka
mazingira mazuri kwa wakulima kwa kuongeza thamani ya zao la muhogo.
Pamoja na mradi huo mbio za Mwenge wa Uhuru ulifanikiwa
kutembelea jumla ya miradi nane (8) yenye thamani ya Bilioni 2.18 katika Wilaya ya Pangani Agosti 12, 2014 ikiwa ni pamoja na kuweka jiwe la msingi
katika ujenzi wa Daharia ya wananfunzi wa chuo cha Ufundi Stadi St. Marys’
Vocational Training Centre, kukagua shamba la ufugaji nyuki kwa kikundi cha Ebeneezer.
Miradi mingine ni uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya , SACCOS ya Vijana
na Chama cha kuweka na kukopa cha Wafugaji na kufungua mradi wa maji Kwakibuyu ambao utanufaisha jumla wa wakazi
wapatao 3,733 ambao ni sawa na asilimia 7% ya wakazi wote wa Wilaya ya Pangani.
Kwa upande wa sekta ya utalii, Bi. Rachel Kassanda alifanikiwa kuzindua hotel ya Saadan Park ambao imejengwa katika kijiji cha Mkwaja na
ipo pembenzoni mwa hifadhi ya Saadan ambayo ni hifadhi pekee duniani
inayopakana na bahari.
Jengo
la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani
lililozinduliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Bi.
Rachel Stephen Kassanda
Bi. Kassanda akijiandaa kumtwisa ndoo ya maji mwanakijiji wa Kwakibuyu wakati
wa ufunguzi wa mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 540,097,52 kupitia programu ya maji
safi wa mazingira vijiji 10. ( RWSSP)
Mkimbiza Mwenge kitaifa, Bw. Yusuph Athumani Shesha akipanda mti wa kumbukumbu mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa daharia ya wanafuzi wa chuo cha Ufundi stadi cha St. Mary wenye thamani ya Shilingi 763,000,000/=
0 comments: