Watanzania watakiwa kuienzi Amani iliyopo Nchini

 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Bi. Rachel Stephen Kassanda akizindua mradi wa Shule ya Awali na Msingi ya Prince and Princess iiyopo eneo la Kange Jijini Tanga



 Halmashauri ya Jiji la Tanga imetoa mikopo ya shilingi milioni sitini (60,000000) kwa vikundi vya VIKOBA vya akina mama ili kusaidia katika uendeshaji wa shughuli za maendeleo . Hii ni asilimia tano ya mapato yake ambayo hutengwa kwa akina mama
  Bw. Seston Fokas Kengele, Msimamizi wa kituo cha umeme kange akitoa ufafanuzi wa mradi wa umeme Kange  kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Bi. Rachel Stephen Kassanda ambao umegharimu dola za kimarekani 3,198,735 ambayo ni takribani shilingi za kitanzania 5,277,912,750 na kufadhiliwa na serikali ya Marekani.
 Clabu ya watoto ya Wapinga Rushwa kutoka shule za Tanga wakipokea zawadi kutoka kwa kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa bi. Rachel Kassanda mara baada ya kupata taarifa ya shughuli za klabu hiyo ambazo ni pamoja na kutoa elimu kwa umma juu ya madhara ya rushwa kupitia sanaa mbalimbali
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Bi. Rachel Kassanda akichoma na kuteketeza  makokoro ambayo hutumika kwa uvuvi haramu katika viwanja vya usagara jijini Tanga ulipokesha  Mwenge wa Uhuru
 Baadhi ya shughuli za maendeleo zilizokaguliwa wakati wa mkesha wa mwenge

 Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Bi. Rachel Stephen Kassanda akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi za Kitanzania   Milion Sitini kwa Kikundi cha Kikoba  fedha ambayo imetolewa na  Halmashauri ya Jiji la Tanga

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bi. Rachel Kassanda amewaasa Watanzania kuenzi amani iliyopo nchini na kuilinda kwa gharama yoyote kwa kutoruhusu mtu awaye yote kuivuruga.
Kauli hiyo ameitoa  juzi (Agosti 10)akiwakilisha  ujumbe wa Mwenge wa uhuru wakati akihutubia wananchi mara tu baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa maji Pongwe katika jiji la Tanga  wenye thamani ya  shilingi za Kitanzania2,037,954,777.00.
“Tusikubali kurubuniwa na watu wanaopenda kuidhoofisha historia yetu ya nchi ambayo inaenzi upendo, mshikamano amani na upendo . Wananchi tutambue kwamba hakuna mtu atakayeruhusiwa kuikanyaga historia ya nchi hii”
Pia ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kupiga kura za maoni ili kujipatiaKatiba mpya ya nchi wakati muda mwafaka ukifika na kuacha tabia ya kutafuta vurugu ambazo haziwezi kumsaidia Mtanzania.
Mradi huo wa maji unajumuisha vijiji vitano vya Marungu, Geza, Kirare, Mapojoni na Mwarongo na unatekelezwa  na Halmashauri ya Jiji la Tanga kupitia program yake ya Maendeleo ya Sekta ya Maji ambapo utanufaisha jumla ya wananchi 12,375. Hii itasaidia kupandisha upatikani wa maji kwa asilimia 99% tofauti na hali ya sasa ya asilimia 76%.

Sambamba na mradi huo Mwenge wa Uhuru umefanikiwa kutembelea jumla ya miradi  ya maendeleo sita (6)  yenye thamani ya shilingi za Kitanzania 12,516,705,798 katika Wilaya ya Tanga. Aidha Mwenge wa Uhuru umezindua miradi mitatu , kuweka mawe ya msingi miradi miwili na kukagua mradi mmoja.
Akitoa taarifa ya upimaji wa ugonjwa wa Ukimwi kwa hiari uliofanyika wakati wa mkesha wa Mwenge wa Uhuru  ,Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Halima Dendego amesema kuwa jumla ya wanachi 1500 wamejitokeza kupima ugonjwa huo na maambukizi  sawa na asilimia 2% jambo ambalo amewaasa wakazi wa Tanga kuendeleza Mapambano dhidi ya ugonjwa huu hatari


Written by

0 comments: