Madiwani Lushoto wahimizwa usimamizi mzuri wa Ukusanyaji wa mapato
Serikali imehimiza usimamizi bora wa ukusanyaji mapato
katika Halmashauri za Wilaya ya Lushoto ili wananchi waweze kunufaika na mapato ya Wilaya yao. Hayo
yamesemwa na Mhe. Chiku Gallawa, Mkuu wa Mkoa wa Tanga wakati wa baraza la
Madiwani lililofanyika katika Ukumbi wa ofisi za Halmashauri ya Mji Lushoto.
Mhe. Gallawa amesema kuwa ni dhamana ya kila kiongozi
kuhakikisha kuwa ukusanyaji wa mapato unasimamiwa vizuri ili Halmashauri ziweze
kupata mapato ya kujiendesha shughuli zake na
hatimaye kuleta maendeleo kwa wananchi na kuwezesha kufikia lengo la Mkoa la Kuinua kipato cha mkazi mmoja mmoja cha Sh millioni moja na nusu kwa mwaka.
Wakitoa maamuzi wakati wa baraza, Madiwani
wamekubaliana kuwa Halmashauri zitoe mafunzo ya taratibu za manunuzi kwa
watendaji wa kata ili kuwawezesha kusimamia vizuri masuala yote ya manunuzi
katika kata zao.
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Majid Mwanga akichangia hoja wakati wa baraza la Madiwani
Sehemu ya Madiwani wakisikiliza kwa makini hoja za baraza
0 comments: