Wajasiriamali Wenye Watoto Walemavu Wafundwa


Wajasiriamali wanawake wenye watoto walemavu wa viungo kutoka Kata 24 za Halmashauri ya jiji la Tanga wakifundishwa namna ya kutengeneza sabuni ya unga na ya maji na Mtaalamu,  Bi. Mise Mushi (katikati) mafunzo yaliyoendeshwa kwa siku  moja na kufadhiliwa na kituo cha watoto wenye ulemavu wa viungo (YDPC) cha Mjini Tanga
Wajasiriamali wanawake wenye watoto walemavu wa viungo kutoka kata 24 za halmashauri ya jiji la Tanga, wakigawana sabuni ya maji waliotengeneza wenyewe baada ya kupata mafunzo ya siku tatu yaliyoendeshwa na kituo cha watoto wenye
ulemavu wa viungo cha YDPC cha mjini Tanga jana.
Wajasiriamali wanawake wenye watoto walemavu kutoka kata 24 za halmashauri ya jiji la
Tanga wakipata mafunzo ya kutengeneza batiki kutoka kwa mwalimu, Mise Mushi
na kuendeshwa na kituo cha walemavu wa viungo cha YDPC cha mjini Tanga jana.


WAJASIRIAMALI wa kazi za mikono kutoka kata 24 za Halmashauri ya jiji la Tanga wametakiwa kuwa wabunifu wa kazi zao ili kuweza kutambulika na kupata masoko ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika ufungaji wa mafunzo ya wajasiriamali wanawake wenye watoto walemavu jana yalioendeshwa na kituo cha Youth with Disabilities Community Program (YDCP), Mratibu wa kituo hicho, William Hendry, aliwataka kuyafanyia kazi mafunzo hayo ili kuweza kujikwamua kimaisha.

Mafunzo hayo ya kutengeneza batiki, chakula cha kuku pamoja na sabuni ya unga na ya maji yaliendeshwa kwa siku tatu na mkufunzi, Mise Mushi na kuvishirikisha vikundi mbalimbali vya wanawake wenye watoto walemavu.


“Nawaomba ujuzi huu mulioupata kwa kutengeneza batiki na sabuni na mengineyo uwe msaada kwenu na kwetu sisi tulio nje----nadhani mmepewa utaalamu wa bure hivyo sasa ni nyinyi kuutokomeza umasikini majumbani” alisema.

“Lengo la kituo hiki kuona mzazi akiwathamini watoto yatima na si  kuona kama ni sababu ya mtoto wake kukosa elimu na huduma muhimu---ni wajibu wa kila mmoja kuutumia vyema ujuzi alioupata” alisema Hendry.

Alisema mafunzo hayo yatawawezesha kila mmoja kujikwamua kimaisha na kuweza kujitangaza katika masoko ya ndani na nje katika maeneo yao na hivyo kuwataka kuzitumilia mbinu hizo na kuwa ukombozi katika maisha yao.

Akizungumzia mafunzo hayo, mjasiriamali kata ya Mabawa, Sakina Rajab, alisema mafunzo hayo ambayo yamemuwezesha kujua kutengeneza sabuni na kanga aina ya batiki yataweza kubadilisha maisha yake.

Alisema awali hakuamini kuwa ataweza kujua kutengeneza bidhaa hizo ambazo zimekuwa zikitumika majumbani kila siku na kuamini kuwa pesa ya kuweza kujikimu na ugumu wa maisha yake yanaweza kuondoka.

“Sikuwa na ndoto kama siku moja nitakuwa mtaalamu wa kutengeneza sabuni na batiki---hii kwangu ni mapinduzi na mageuzi makubwa katika maisha yangu” alisema Sakina.

Sakina aliwataka wanawake kujingiza katika vikundi vya ujasiriamali na kuweza kupata mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali na kuepuka vishawishi ambavyo vitaweza kumuharibia mtu maisha yake.






Written by

0 comments: