Mwenge Wa Uhuru 2014 Kuzindua Miradi 61 Yenye Thamani Ya Bilioni 27 Mkoani Tanga
Mkoa wa Tanga leo umepokea Mwenge wa
Uhuru uwanja wa ndege wa Tanga ukitokea Mkoa wa Kusini Pemba katika ambapo utapata fursa ya kutembelea,
kuzindua na kuweka mawe ya msingi miradi 61 yenye thamani ya shilingi za Kitanzania 27,349,223,704/= (Billion isirini na saba, milioni mia tatu
arobaini na tisa, laki mbili na ishirini na tatu na mia saba na nne) katika
Wilaya zake nane ambazo ni Tanga, Mkinga, Muheza, Pangani, Handeni, Kilindi,
Korogwe na Lushoto.
Ujumbe wa Mwenge mwaka huu ni Katiba ni Sheria Kuu ya
Nchi wenye Kauli mbiu yenye kauli mbiu”
Jitokeze kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba Mpya” . Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba ,Meja
Mst Juma Kasim Tindwa akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mhe. Chiku Gallawa , Mkuu
wa Mkoa wa Tanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Pemba Kusini Bi. Hanuna Ibrahim Masud akisoma taarifa ya makabidhiano ya Mwenge kwaMkoa wa Tanga
Bw. Salum M. Chima , Katibu Tawala Mkoa wa Tanga
akisoma taarifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru
Baadhi Viongozi ngazi za Mkoa na Taifa na wananchi
wakati wa mapokezi ya Mwenge wa uhuru
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa akikabidhi Mwenge
wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Halima Dendego ikiwa ni Wilaya ya
kwanza kukimbiza Mwenge wa Uhuru kwa Mkoa wa Tanga
0 comments: