Wakulima 3600 Kunufaika Na Mradi Wa Matrekta Makubwa Handeni

 Halmashauri ya Wilaya ya Handeni  kupitia Kauli mbiu ya Taifa ya Matokeo Makubwa Sasa imeendelea kuhamasisha matumizi ya matrekta makubwa ili kukipatia kilimo tija na kuwanufaisha wakulima.


Hayo yamethibitishwa Agosti 13 katika Kata ya Kwamsisi wakati Kiongozi wa mbio za Mwenge Bi Rachel Kassanda amefanikiwa kuzindua matrekta makubwa sana (7) yenye thamani ya shilingi milioni 314,639,976.25 ambayo yatanufaisha wakulima wapatao 3600 kutoka vijiji saba vya Kwangwe,Komsaka, Kwachaga, Tuliani,Madara, Chogo, Mkata Mashariki na Sundeni.

Akizungumza wakati akitoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru Bi Kassanda  ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kubeza juhudi za Serikali kwa kuwataka kutumia fursa zinzoletwa na serikali katika kujiletea maedneleo badala ya kukaa na kulalamika.

Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imewapatia Maafisa Ugani pikipiki tisa (9)zenye thamani ya shilingi milioni 22,680,000 kwa lengo la kuboresha mazingira yao ya kazi. Mwenge wa Uhuru umetembelea miradi 10 ya maendeleo Wilayani humo yenye thamani ya shilingi za Kitanzania Bilioni 2.1 mnamo Agosti 13.
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Mhingo Rweyemamu akisoma taarifa ya Wilaya kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2014, Bi. Rachel Stephen Kassanda mara bada ya Mwenge wa uhuru kuwasili Wilayani humo

 Elizabeth Tumaini kutoka kikundi cha Ujamaa Kwenjugo Mashariki akipokea hudi ya fedha ya kikundi chake. Halmashauri ya Handeni imefanikiwa  kutoa sh. Milioni 40,000,000/= ambayo ni asilimia tano ya mapato ya ndani ya makusanyo kwa ajili ya vijana na wanawake. Milioni 30,000,000 zimekopeshwa kwa SACCOSS ya vijana na milioni 10,000,000 zimekopeshwa kwa vikundi 9 vya akina mama
 Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Bi. Rachel Kassanda akiweka jiwe la msingi jingo la  zahanati  Kijiji cha mkalamo. Mradi huu  hadi kukamilika kwake utagharimu kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 85,000,000/=

 Pikipiki tisa (9)zenye thamani ya shilingi milioni 22,680,000 zenye  lengo la kuboresha mazingira yao ya kazi kwa mafisa Ugani
Bi. Rachel Stephen Kassanda , Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa akizugumza na wawakilishi kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mara baada ya ya kutembelea bada lao.


Written by

0 comments: