Polisi Mkoani Tanga Yakamata Noti Bandia
Watu watatu wanaosemekana kujishuhusisha
na biashara ya uuzaji wa noti bandia Mkoani Tanga wamekamatwa na Jeshi la
Polisi Mkoani hapa wakiwa na dola za kimarekani zenye thamani ya 11200 ambazo
ni sawa na shilingi milioni 20 za Kitanzania .
Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Tanga, Fresser Kashai aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa
watuhumiwa hao walikamatwa Novemba 17 mwaka huu saa saba na nusu eneo la
barabara ya kumi na sita Kata ya Ngamiani wilayani Tanga wakati kwenye
harakati za kuziingiza kwenye mzunguko.
Alisema kuwa watuhumiwa hao
walikamatwa na Polisi wakiwa kwenye gari lenye Chasis namba JLg 100037726
ambazo ni wakazi wa Jijini Dar es Salaam wakiwa na noti hizo bandia ambazo
walikuwa wamezificha .
Aliwataja watuhumiwa wanaoshikiliwa na
Jeshi hilo kuwa ni Julius Kanza(30),kabila Mchaga na Mkazi wa Ubungo,Kenedy
Binagi(35) mkazi wa Sinza na wa tatu ni Ramadhani Saddy(33) kabila Muha
na mkazi wa Mwenge.
Kamanda Kashai alisema kuwa baada ya
watuhumiwa hao kukamatwa walikiri kuhusika na biashara hiyo ambapo wanatarajiwa
kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili mara baada ya upelekezi wa
awali kukamilika.
Wakati huo huo,Jeshi la Polisi Mkoani
Tanga linaendesha msako mkali wa kuwatafuta wahusika wa matukio ya mauaji ya
Mkulima mmoja yaliyotokea Kijiji cha Nyadigwa Kata na Tarafa ya Kimbe wilayani
Kilindi.
Kamanda Kashai alisema kuwa tukio
hilo la mauaji hayo lilitokea Novemba 18 mwaka huu majira ya saa kumi na moja
na dakika arobaini na tano katika eneo la kijiji cha Vyadigwa Kata ya Kimbe
wilayani humo.
Akizungumzia tukio hilo,Kamanda
Kashai alisema mkulima wa Vyadigwa alikutwa porini akiwa amejeruhiwa maeneo ya
utosini kwa kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana hali iliyomsababishia
kifo chake.
0 comments: