Uzinduzi Wa Kuhamasisha Wananchi Kujiunga Na Mfuko Wa Afya Ya Jamii(CHF) Wilaya ya Muheza, Zaidi Ya Kaya 65 Zajiunga hapo kwa papo
Mkuu wa Wilaya ya Muheza
Mhe. Subira Mgalu akisisitiza jambo wakati uzinduzi wa kuhamasisha wananchi
kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii(CHF) kwenye kata ya Potwe wilayani Muheza uliofanyika leo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama
390 walihamasiska na kujiunga hapo kwa papo
Mmoja wa Maafisa
kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya(NHIF) akihamashaa kwenye zoezi hilo na kuamua kuwalipia wanafunzi wa shule
za msingi wapatao 80 kwenye Kata ya Potwe wilayani Muheza wanaoishi kwenye
mazingira magumu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga
na mfuko wa afya ya Jamii (CHF) wilayani humo ambapo zoezi hilo linaendelea kwa
muda wa siku kumi
Afisa wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF)kutoka Makao Makuu Isaya Shekifu wa pili kulia akifuatilia
uandikishwaji wa wanachama wapya wa mfuko wa afya ya Jamii(CHF) leo (Jana) wakati wa
uzinduzi wake uliofanyika Kata ya Potwe Wilayani Muheza wa kwanza kulia ni Afisa Tabibu wa Zahanati ya Potwe
kulikofanyika uzinduzi huo,Dr.Swalehe Mudhihiri ambapo zaidi ya kaya 65 zenye
wanachama 390 zilifanikiwa kujiunga
Wananchi kutoka sehemu mbalimbali kwenye Kata ya Potwe
wilayani Muheza wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza ambaye hayupo pichani
wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya
jamii(CHF) Picha & stori na Osca Assenga- Muheza
0 comments: