Kamati Ya Bunge Ya Kilimo, Maji Na Mifugo Yaonya Uharibifu Wa Mazingira katika Vyanzo vya Maji
Uchimbaji
wa madini katika chanzo cha maji cha mto Zigi uliopo eneo la Amani Wilaya ya
Muheza umeendelea kuleta madhara makubwa
kwa kusababisha kupungua kwa maji ambayo awali yamekuwa msaada mkubwa kwa
wakazi wa Tanga.
Hayo yamebainika wakati wa
ziara ya siku moja ya Kamati ndogo ya
Bunge ya Kilimo, Maji na Mifugo ilipotembelea katika eneo hilo mwanzoni mwa wiki ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa miradi ya maji
katika Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara
Akizungumza mara baada ya
kusomewa taarifa ya maendeleo ya chanzo cha maji ya mto Zigi, Mwenyekiti wa Kamati
ndogo ya Bunge Mhe. Moshi Selemani Kakoso ameutahadharisha umma kuwa muda
uliobaki si wa kulalamikia madhara bali kila mwananchi ana jukumu la kuchukua hatua
katika utunzaji wa mazingira.
“Wafichueni waharifu wa
mazingira kwani waharibifu sio wageni bali ni miongoni mwa wakazi wa eneo
husika” alisisitiza Mhe. Kakoso
Vile vile wito umetolewa
kwa Uongozi wa Mamlaka ya Maji Tanga kuhakikisha kuwa wanabuni miradi ya
maendeleo ambayo ni endelevu ili kuwawezesha wananchi kuachana na uchimbaji wa
madini katika eneo la chanzo cha maji.
Wakijibu hoja ya Miradi ya
mendeleo, Mamlaka ya maji Tanga imesema tayari ipo miradi mbalimbali ambayo
inaendeshwa na Mamlaka hiyo na kiasi cha shilingi millioni 100 zimeshatengwa
kwa mwaka 2014/15 kwa ajili ya kuboresha maisha ya wakazi ambao wanaishi eneo
karibu na chanzo cha maji cha mti Zigi.
Nao wananchi wakizungumza
wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Sangarawe ambacho kipo karibu na hifadhi ya
taifa ya Amani, wameiomba serikali kuona uwezekano wa kuboresha barabara ili kusaidia usafirishaji wa mazao
kwenda muheza mjini.
Naye mwenyekiti wa
Halmashauri ya Muheza amewakumbusha wananchi kuwa tayari serikali imeshaanza
mchakato wa kuendeleza barabara hiyo na kwa sasa iko katika kiwango cha
changalawe na jitihada zinafanyika ili barabara hiyo iweze kuwekwa katika
kiwango cha lami katika siku za usoni.
Katibu
Tawala Msaidizi kutoka ofisi ya Mkuu wa
Mkoa Tanga Eng. Ephraim Minde akifafanua jambo mara baada ya Kamati ya Bunge na wawakilishi kutoka Wizara ya Kilimo kuwasili ofisi ya
Mkuu wa Wilaya ya Muheza
Mjumbe wa Kamati ya Bunge
Mhe Subira K. Mgalu ambaye pia ni Mkuu
wa Wilaya ya Muheza akitoa ufafanuzi na kuonyesha uharibifu unaoendelea katika
eneo la Chanzo cha maji cha mto Zigi eneo la Amani Wilaya ya muheza mara baada ya kutembelea eneo la Sangarawe. Kulia kwake ni mjumbe wa Kamati Vrajlal Son.
Taswira ya sasa ya baadhi ya eneo la Sangarawe baada ya uchimbaji wa madini usio rasmi unaofanywa na vijana wa
eneo hilo
Bw.
Shaban Hamis Mzava- Meneja wa Mamlaka ya Maji Wilaya ya Muheza akisoma taarifa
ya mradi wa Maji Kijiji cha Ubembe
Wilaya ya Muheza mara baada ya Kamati ya Bunge ya kilimo, Maji na Mifugo kutembelea Mradi huo.
Kamati ikitembelea mradi huo
Mradi wa maji Kijiji cha Ubembe Wilaya ya Muheza
0 comments: