Serikali Yasema Zoezi La Kupigia Kura Katiba inayopendekezwa Liko Pale Pale
Serikali imewahikikishia watanzania
kuwa zoezi la uandikishwaji wa wapiga kura katika daftari la kudumu kwa mfumo
wa kieletroniki BVR litafanyika kwa ufanisi na ndani ya wakati uliopangwa.
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Mhe.
Mizengo Pinda Bungeni leo wakati akijibu swali la kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni
Mhe. Freeman Mbowe kuhusu uhakika wa zoezi hilo na pia ameuhakikishia umma kuwa
vifaa vinavyotarajiwa kuletwa vina ubora
mara ya mbili ya vilivyoletwa mwanzo kwa ajili ya zoezi la majaribio hilo.
Mhe. Pinda amewataka wananchi wasiwe
na wasiwasi bali wajiandaa vyema kwa kuwa zoezi la upigaji kura kwa ajili ya katiba
mpya litafanyika katika tarehe iliyopangwa .
Vile vile Mhe. Pinda amesisitiza kuwa endapo tume itaona kuwa zoezi hilo haliwezekani kwa sababu yoyote ile, itatoa taarifa serikalini na serikali iko tayari kubadili maamuzi.
Zoezi la kupiga kura ya maoni linatarajiwa kufanyika April 30 mwaka huu .
0 comments: